MCHUNGAJI AFUNGWA KWA UBAKAJI!!!!
Kiongozi
wa kanisa moja nchini Zimbabwe amehukumiwa kifungo cha miaka 40 jela
kwa kosa la kuwabaka wanawake watatu na kukutwa na vifaa vya kuchochea
kujamiiana.
Kiongozi
huyo, Martin Gumbura (57) wa Kanisa la RMG Independent End Time Message
alitiwa hatiana katika makosa manne ya ubakaji kwenye mahakama ya mjini
Harare. Gumbura ana wake 11 na watoto 30 na aliiambia mahakama kwamba
alikuwa akitarajia kupata watoto 100 katika maisha yake.
Wake
zake wote walikuwa wakihudhuria mahakamani hapo wakati wa kesi hiyo na
walikuwa wakijumuika na watu wengine waliokuwa wakihudhuria makahamani
hapo hadi siku hukumu ilipotolewa.
Alihukimiwa
kifungo cha mika 50 jela lakini miaka 10 imepungizwa katika adhabu hiyo
baada ya kuonyesha tabia njema wakati wa kesi hiyo.
Hukumu
nyingine ya kifungo cha miaka minne jela kwa kukutwa na vifaa vya
kuchochea kujamiiana itatumikiwa sambamba na hukumu hiyo ya kifungo cha
miaka 40. Waendesha mashtaka waliiomba mahakama kwamba Gumburu anatakiwa
ahukumiwe kifungo cha miaka 25 jela kwa kila kosa, lakini hakimu
alieleza kwamba hana mamlaka ya kutoa hukumu ya kifungo cha muda mrefu
namna hiyo.
Hakimu huyo alimwelezea Gumbura kama mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo ambaye amekuwa akiwaghilibu waumini wa Kanisa hilo.
“Mahakama
imejaribu kutoa adhabu ambayo itawatendea haki wote, malalmikiwa na
walalamikaji. Mtuhumiwa hutu ni kama mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya
kondoo,” alisema.
“Msingi
wa huduma ya Kanisa ni kumwabudu Mungu na si kuzini na mabinti na
wanawake na kuwatishia kwamba kwa kutofanya hivyo watapatwa na balaa,”
aliongeza hakimu huyo.
Alisema
ni wajibu wa wachungaji na wasimamizi wa kanisa kujua kuhusu madhila
yanayowakumba waumini wao, pia kujua udhalilishaji na unyanyasaji wa
kijinsia unaowakumba wanawake na kutafuta namna ya kuukemea.
Awali
Gumbura alikuwa akikabilwia na mashtaka tisa ya kuwalaghai na kuwabaka
wanawake sita lakini alifutiwa mashtaka manne yaliyowahusisha wanawake
watatu kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.
Hivi
karibuni, mtu mwingine mjini Harare alihukumiwa kifungo cha miaka 290
jela kwa kosa la kuwadhalilisha na kuwabaka wanawake 13. Mtu huyo,
Thomas Chirembwe (30) alitiwa hatiani kwa makosa 21 ya ubakaji na
ujambazi wa kutumia silaha baada ya mfululizo wa matukio yaliyoutikisa
mji wa Harare.
Kwa
mujibu wa takwimu za polisi, zaidi ta watoto 400 walibakwa na wanawake
392 walinyanyaswa kijinsia mwaka 2013, ambapo wanawake walibakwa wakiwa
njiani na watoto wengi walibakwa na majirani au watu wao wa karibu.
0 comments: