Showing posts with label MATUKIO. Show all posts

LULU ATINGA MAHAKAMA KUU DAR HAPO JANA KUSIKILIZA KESI YAKE

0 comments



Elizabeth Michael ‘Lulu’.
STAA wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametinga ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiambatana na msanii maarufu wa filamu Bongo, Mahsein Awadh 'Dk. Cheni' tayari
kusikiliza kesi yake inayomkabili juu ya kifo cha marehemu Steven Kanumba!
Lulu amewasili mahakamani hapo bila wasiwasi wowote na kwenda kukaa akisubiri kesi yake kuanza.

FUMANIZI KUBWA!!!!! MDADA APIGWA NA KUKATWA VIDOLE BAADA YA KUNASWA AKISALITI NDOA:

0 comments
clip_image003Mwanamke mmoja apigwa vibaya na mume wake hadi kukatwa vidole baada Mumewe kugundua kuwa anamsaliti,
Tukio hilo lilitokea majira ya jioni jamaa huyo aliporudi kazini na kumkosa mke wake baada ya kumpigia simu alisema yuko kwa rafiki yake, jamaa aliwasha gari na kufika hadi kwa huyo rafiki yake, alipofika alimpigia tena simu na kumuambia nimefika mke wangu niko hapa nje , mwanamke alisema kuwa wametoka kidogo yeye na huyo rafiki yake ila watarudi muda sio mrefu, jamaa alimuuliza mke wake mko wapi ili niwafuate huko sasa hivi mwanamke alieleza kwamba wako bekari wanaangalia nini cha kununua, jamaa akamuambia mke wake nisubiri hapo hapo nakuja usiondoke,..
alipofika eneo hilo aliloelekezwa hakukuwa na bakery alijaribu kuulizia hakufanikiwa kupata bekari, alimpigia tena mke wake simu na kumuuliza mbona maeneo haya hakuna bakery? mwanamke akajibu nimeshatoka huko niko njiani sasa hivi nakaribia kwa rafiki yangu.

Jamaa alirudi tena kwa hasira na kufika pale kwa huyo rafiki yake. akamkuta mke wake yuko pale akamuomba warudi nyumbani. Walivyofika nyumbani jamaa akamuuliza mke wake ulikuwa wapi? mwanamke akajibu kwa rafiki yangu, huku akiogopa na kuonekana ana wasi wasi.
Alichukua simu yake meseji ya kwanza aliyokutana nayo ni ya mwanaume ikisema "nipo kwangu mpenzi mbona hufiki" jamaa alianza kushusha kipigo cha mbwa mwizi hadi kufikia kumkata mwanamke huyo vidole na kumuumiza vibaya

     TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI!!!

MCHUNGAJI AFUNGWA KWA UBAKAJI!!!!

0 comments

Kiongozi wa kanisa moja nchini Zimbabwe amehukumiwa kifungo cha miaka 40 jela kwa kosa la kuwabaka wanawake watatu na kukutwa na vifaa vya kuchochea kujamiiana.
Kiongozi huyo, Martin Gumbura (57) wa Kanisa la RMG Independent End Time Message alitiwa hatiana katika makosa manne ya ubakaji kwenye mahakama ya mjini Harare. Gumbura ana wake 11 na watoto 30 na aliiambia mahakama kwamba alikuwa akitarajia kupata watoto 100 katika maisha yake.
Wake zake wote walikuwa wakihudhuria mahakamani hapo wakati wa kesi hiyo na walikuwa wakijumuika na watu wengine waliokuwa wakihudhuria makahamani hapo hadi siku hukumu ilipotolewa.
Alihukimiwa kifungo cha mika 50 jela lakini miaka 10 imepungizwa katika adhabu hiyo baada ya kuonyesha tabia njema wakati wa kesi hiyo.
Hukumu nyingine ya kifungo cha miaka minne jela kwa kukutwa na vifaa vya kuchochea kujamiiana itatumikiwa sambamba na hukumu hiyo ya kifungo cha miaka 40. Waendesha mashtaka waliiomba mahakama kwamba Gumburu anatakiwa ahukumiwe kifungo cha miaka 25 jela kwa kila kosa, lakini hakimu alieleza kwamba hana mamlaka ya kutoa hukumu ya kifungo cha muda mrefu namna hiyo.
Hakimu huyo alimwelezea Gumbura kama mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo ambaye amekuwa akiwaghilibu waumini wa Kanisa hilo.
“Mahakama imejaribu kutoa adhabu ambayo itawatendea haki wote, malalmikiwa na walalamikaji. Mtuhumiwa hutu ni kama mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo,” alisema.
“Msingi wa huduma ya Kanisa ni kumwabudu Mungu na si kuzini na mabinti na wanawake na kuwatishia kwamba kwa kutofanya hivyo watapatwa na balaa,” aliongeza hakimu huyo.
Alisema ni wajibu wa wachungaji na wasimamizi wa kanisa kujua kuhusu madhila yanayowakumba waumini wao, pia kujua udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia unaowakumba wanawake na kutafuta namna ya kuukemea.
Awali Gumbura alikuwa akikabilwia na mashtaka tisa ya kuwalaghai na kuwabaka wanawake sita lakini alifutiwa mashtaka manne yaliyowahusisha wanawake watatu kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.
Hivi karibuni, mtu mwingine mjini Harare alihukumiwa kifungo cha miaka 290 jela kwa kosa la kuwadhalilisha na kuwabaka wanawake 13. Mtu huyo, Thomas Chirembwe (30) alitiwa hatiani kwa makosa 21 ya ubakaji na ujambazi wa kutumia silaha baada ya mfululizo wa matukio yaliyoutikisa mji wa Harare.
Kwa mujibu wa takwimu za polisi, zaidi ta watoto 400 walibakwa na wanawake 392 walinyanyaswa kijinsia mwaka 2013, ambapo wanawake walibakwa wakiwa njiani na watoto wengi walibakwa na majirani au watu wao wa karibu.

MAMBO HADHARANI: MAUAJI YA WAFARANSA WALIOTUPWA KWENYE KISIMA CHA MAJI ZANZIBAR

0 comments
Zanzibar Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji (KZU) na Polisi wamefanikiwa kuvunja zege lililokuwa limejengwa kufunika kisima walichotupwa raia wawili wa Ufaransa, baada ya kuuawa na kupata sehemu za miili yao ikiwamo fuvu la kichwa.
Aidha, siri za mauaji hayo zimeanza kuvuja, ikielezwa kwamba waliotekeleza unyama huo walilenga kupora nyumba na kiasi kikubwa chafedha.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi na Makosa ya Jinai Zanzibar (DCI) Yussuf Illembo, alisema kuwa hadi jana mchana, mifupa miwili ya mapaja, fuvu la kichwa na miwili ya mbavu imepatikana kutoka ndani ya kisima hicho.
Alisema kwamba Kikosi Kazi cha Uokoaji kinaendelea kufanya kazi eneo hilo la Matemwe lililopo Shehia ya Kaskazini, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
“Kazi bado ni ngumu, tunaendelea kuzamia ndani ya kisima na itakapokamilika tutatoa taarifa. Tuacheni kwanza tufanye kazi hii nzito na ngumu kwa wakati huu,” aliomba DCI Illembo.
Zoezi hilo lilifanyika huku likishuhudiwa na ofisa mmoja wa Ubalozi wa Ufaransa nchini na kuelezwa kuwa marehemu hao walinunua eneo la ardhi na nyumba kwa Sh150 milioni kwa kutumia jina moja la mzawa wa Zanzibar, kutokana na sheria kutoruhusu wageni kumiliki ardhi visiwani humo.
Watu hao, Francios Chererobert Daniel, aliyekuwa mtumishi mstaafu wa ngazi za juu wa Serikali ya Ufaransa na mkewe Brigette Mary, walipotea tangu Desemba 27 mwaka jana.
Baadaye taarifa za kupotea kwa watu hao zilifikishwa Polisi ndipo msako wa kuwatafuta ulipoanza na baadaye kugundulika kuwa, kuna watu wameuawa na miili yao kutupwa katika kisima cha maji kilichopo ndani ya ua wa nyumba hiyo.
Hata hivyo, baadhi ya waokoaji na mashuhuda wa tukio hilo, waliliambia gazeti hili kwamba sehemu hizo za mwili zinazosadikiwa kuwa za Wafaransa hao, zimefukuliwa baada ya kazi kubwa ya kuvunja zege kwa kutumia mashine maalumu inayofanywa na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wakazi wa eneo hilo.
“Tumefanikiwa kutoa sehemu ya miili, imehifadhiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja,” alisema mmoja wa mashuhuda aliyeomba jina lake lisitajwe.
Alisema kuwa kazi ya kuvunja zege hilo ilikuwa ngumu, walilazimika kuwachukua vijana wengine raia wa kawaida ili kuifanikisha.
Akielezea mazingira waliyokutana nayo chini ya kisima walichotupwa Wafaransa hao, alisema kuwa baada ya zege kuvunjwa walikuta nguo nyingi zimejazwa chini yake na juu yake kujengwa zege hilo kabla ya kumwagwa saruji isiyochanganywa kitu ili kufunika kisima kwa lengo la kupoteza ushahidi.
Hata hivyo, vyanzo vya habari vinaeleza kuwa zoezi hilo lililazimika kusitishwa kutokana na sehemu ya chini ya kisima kupita mkondo wa maji ya bahari, hivyo kulazimika kutafuta mashine ya kuvuta maji.
“Kazi hiyo ikiweza kufanyika ndipo tutakapoweza kwenda katika kina kirefu zaidi cha kisima hicho ili kukusanya mifupa. Tukipata idadi ya mifupa na mafuvu yote, tutaweza kujua waliouawa ni wangapi,” kilieleza chanzo kimoja.
Sheha wa Shehia ya Matemwe Kusini, Denge Khamis Silima alisema kuwa wanapata faraja kuona zoezi hilo limepata mafanikio tofauti na siku ya kwanza na kwamba kazi hiyo inaendelea kufanyika kwa umakini huku akiitaka Serikali kuwapatia vifaa waokoaji ili kufanikisha kazi hiyo.

Siri ya mauaji
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa siri ya mauaji hayo ni baadhi ya watu kutaka kupora nyumba, waliyokuwa wakiishi Wafaransa hao pamoja na fedha zinazodaiwa walikuwa nazo raia hao wa kigeni wakitaka kununua eneo la kujenga hoteli kwenye ufukwe wa Urowa.
Inelezwa kuwa kabla ya kuingia Zanzibar, Wafaransa hao walifikia Nairobi nchini Kenya ambako inadaiwa kuwa mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini humo aliwashauri kwenda Zanzibar kuishi na kuwekeza.
Taarifa zaidi kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa mazingira ya tukio hilo yanaonyesha kuwa kabla ya watu hao kuuawa, mbwa wao aliyekuwa akifahamika kwa jina la Allan, alipewa chakula chenye sumu na kufa na kwamba sehemu ya mabaki ya chakula hicho yaliliwa na mbwa wa jirani ambaye pia alikufa.
Aidha, mifuko mitupu ya saruji inayosadikiwa kutumika katika ujenzi wa zege la kisima hicho, imeokotwa nyuma ya ukuta wa nyumba hiyo waliyokuwa wakiishi Wafaransa hao. 

EXCLUSIVE : KWELI MZIKI UNALIPA BASI HII NDO NYUMBA ALIYONUNUA MSANII YOUNG DEE MAENEO YA KIMARA. ICHEKI HAPA

0 comments

                                      Star wako Young Dee ameweza kupost picha za Crib yake mpya ambayo ameinunua na kuiweka  katika akaunti yake ya instagram.com na kuweza kusema “When i say i love music this is wats uup!!! Jus bought a crib oohh lord..”
Crib hii ambayo ipo maeneo ya Kimara suka Star wako Young Dee amepiga story na perfecttz.com kwamba mpaka mwezi wa Saba au Nane atakua tayari ameshahamia rasmi kwa sababu ryt now ipo katika matengenezo!


MASKINI WEMA SEPETU...MAJANGA YAZIDI KUMUANDAMA....KUPANDA TENA KIZIMBANI..SOMA ZAIDI HAPA...!

0 comments


MENEJA wa hotel ya Mediteranian iliyoko Kawe Beach jijini Dar es salaam aliyepigwa makofi na kutukanwa na beautiful Onyinye wa bongo movies Wema Isack Sepetu amesema kuwa ameshampata wakili mkubwa wa kumsaidia katika rufaa ya kesi yake na kwamba sasa kesi hiyo itasimamiwa kwa ushirikiano na mabosi wake.
 
Akiongea na Swahilitz meneja huyo ambaye hakuridhika na hukumu ya Wema kutoa laki moja na kumaliza kesi katika mahakama ya mwanza ya Kawe chini ya mheshimiwa Hakimu Bernice Ikanda. "Unajua mara ya kwanza niliambiwa siwezi kushindanan na Wema kutokana na mwanja mkubwa aliokuwa nao lakini nilimuomba Mungu anisaidie kwa hilo kwasababu kwa Mungu hakuhitaji hela, nimesimama kidete na kumuomba Mungu na sasa kesi nairudisha upya kwani wakili niliyempata na wa kizito na ni wa uhakika" alisema meneja huyo. Alifafanua kuwa katika rufaa yake atakuwa sambamba na wakili huyo pamoja na wamiliki wa hotel ya Mediteranian ambao kwa pamoja wameahidi kuhakikisha suala hilo linapatia ufumbuzi yakinifu. Wema alipandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yake na Mheshimiwa Hakimu Bernice Ikanda na kudaiwa kufanya  vurugu kushambulia na kumpiga makofi na kumtukana bwana Goodluck Kayumbu. Hata hivyo katika katika kujitetea alidai kuwa yote yalifanyika kwasababu ya pombe na sio kwa masudi 
Hatua ya bwana Kayumbu kukimbilia rufaa katika kesi ambayo ilishamalizika ni pigo la pili kwa Wema ndani ya mwaka huu kwani hivi karibuni imeelezwa kuwa alikumbwa na mkosi baada ya mahakama ya Ilala kuamuru anyang'anywe gari lake la kifahari aina ya Audi Q7 lenye usajili wa T973 BUJ na kukabidhiwa kwa mmiliki wa gari hilo.

MASKINI JOHARI....“Siwezi kuzungumza vizuri, sauti yangu iko chini sana... nahisi kama inakauka...

0 comments

."

MASKINI! Ndiyo neno linaloweza kumtoka mtu yeyote mwenye mapenzi mema na staa wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ambaye kwa sasa afya yake si ya kuridhisha, Ijumaa lina kila kitu.
Blandina Chagula ‘Johari’.
Johari ni mgonjwa kwa zaidi ya siku tano sasa akiwa mtu wa kwenda hospitali mara kwa mara kwa ajili ya kuendelea na matibabu.

TAARIFA ZA AWALI
Shostito wa karibu na staa huyo alipiga simu chumba cha habari cha gazeti hili, wiki iliyopita akieleza kwamba Johari ni mgonjwa na amekuwa mtu wa kupumzika ndani.


Rafiki huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake alisema: “Najua mtakuwa hamna hii habari, lakini kiukweli Johari anaumwa, jana (Jumanne iliyopita) nilikwenda kwake, hali niliyomkuta nayo kwa kweli nilimhurumia, yawezekana pia ile ishu yake na Ray inamchanganya, ukimuona amepungua, siyo yule unayemjua.”
 
 
Blandina Chagula ‘Johari’.
JOHARI ATAFUTWA
Katika kutaka kujiridhisha, mmoja wa wahariri wa Global Publishers, alimvutia waya Johari Jumanne iliyopita, ambapo alipokea na kuzungumza kwa shida huku sauti ikiwa chini sana.


“Siwezi kuzungumza vizuri, sauti yangu iko chini sana... nahisi kama inakauka. Naumwa sana. Nina fluu,” alisema Johari.
Baada ya mazungumzo hayo, gazeti hili lilipata uhakika kuwa ni kweli Johari ni mgonjwa lakini hakuwa ‘siriazi’ kivile, likachukulia poa. 

HALI YABADILIKA
Siku mbili baadaye, chanzo chetu kilekile cha awali kilipiga tena simu na kutoa taarifa kuwa hali ya Johari ilibadilika ghafla na kwamba alifikishwa hospitalini.

Hata hivyo, alipoulizwa ni hospitali gani amelazwa, alisema hana uhakika lakini alisikia kama amepelekwa AAR ya Sinza. Simu ya Johari ilipopigwa, haikupatikana achilia mbali marafiki zake wa karibu. 

MAPAPARAZI HOSPITALINI
Timu yetu ilifunga safari hadi Hospitali ya AAR (Sinza) na ile nyingine ya Posta na kujaribu kudodosa kama alifikishwa hospitalini hapo, likaambulia patupu. 


STEVE NYERERE AANZA KAZI
Katika kuonyesha kuwa mwenyekiti mpya wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ amedhamiria kuweka umoja na ushirikiano kwa wasanii walio kwenye klabu hiyo kwenye shida na raha, ndiye aliyemtoa Johari hospitalini.


Steve Nyerere aliweka picha kwenye ukurasa wake wa Instergram inayomwonesha Johari akiwa katika hali ya kuugua, huku mkononi mwake akiwa na plasta iliyoonyesha kuwa alitundikiwa drip na kuandika: “Johari haya ndiyo maisha, usijali utapona.” 
MAPAPARAZI NYUMBANI KWA JOHARI
Juzi Jumatano, timu ya waandishi wetu ilifunga safari hadi nyumbani kwa Johari, Ubungo – External, Dar ili kujua hali yake.

Hatua chache kabla ya kufika nyumbani kwake, gazeti hili lilimpigia simu, lakini hakupokea badala yake alilitumia ujumbe mfupi uliosema: “Siwezi kuongea, naomba unitumie meseji, naumwa sana na fluu, naamini nitapona. Nitakutafuta.”
Ijumaa: Nipo na karibu na kwako, nakuja kukuona.
Johari: Sipo nyumbani, nipo hospitalini.
Ijumaa: Hospitali gani?
Johari: AAR. 


UHAKIKA
Pamoja na majibu ya Johari, bado gazeti hili lilitaka kujiridhisha zaidi, halikuishia njiani, lilifika hadi nyumbani kwake ambapo lilipokelewa na kijana wa kiume aliyekataa kutaja jina lake lakini alijitambulisha kama mdogo wake na Johari.


Alipoulizwa kuhusu Johari, haraka alisema: “Dada anaumwa, amekwenda hospitali. Kwa nini msiwasiliane naye kwenye simu?”
POLE JOHARI
 
Kuugua ni sehemu ya maisha Johari. Ni mitihani ambayo binadamu wote tumeumbiwa hivyo jipe moyo, utapona. Mungu aisimamie afya yako, upone haraka – Amina.