LULU AMEKIRI, ALIKUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA KANUMBA, HUU NDO USHAHIDI ALIOUTOA MAHAKAMANI
0 comments
MSANII wa Filamu nchini, Elizabeth Michael'Lulu' ambaye anakabiliwa na
kesi ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, amekiri
kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii huyo na kwamba walikuwa
na ugomvi.
Lulu alikiri hayo leo wakati akisomewa mashitaka yake mbele ya Jaji Rose
Temba wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es salaam ambapo lulu baada ya
kusomewa mashitaka amekana kumuua.
Mbali na kukiri kuwa na uhusiano, pia lulu akikiri kuwa baada ya tukio
alitoka nje ya chumba walichokuwepo na kwenda kumwambia mdogo wake
Marehemu Kanumba, Setti Bosco kuwa marehemu amedondoka.
Akisoma hati ya mashitaka Wakili Mwandamizi wa Serikali, Monica Mbogo,
alidai kuwa Aprili 7, mwaka 2012, Sinza Vatikani, Mkoa wa Dar es salaam,
mshitakiwa alimuua bila kukusudia msanii Kanumba.
Wakili Kombo, alidai kuwa pamoja na mambo mengine, marehemu Kanumba
baada ya kufa, mwili wake ilipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo
majibu yanaonyesha kwamba kifo chake kimesababishwa na uvimbe ndani ya
ubongo.
Upande wa serikali una mashahidi watano pamoja na vielelezo wakati
upande wa utetezi unatarajia kuwa na mashahidi watano na vielelezo.